10 Septemba 2016 - 20:45
Magaidi 100 wa Daesh waangamia magharibi mwa Iraq

Majeshi ya anga ya Iraq yamefanya mashambulio ya anga katika ngome za magaidi wa Daesh katika mkoa wa Anbar nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Iraq yamefanikiwa kupata ushindi mpya dhidi ya magaidi wa Daesh nchini humo, ambapo majeshi ya anga kwakufanya mashambulizi ya anga katika ngome za Daesh ziliopo magharibi mwa mkoa wa Anbar, ambapo kikundi cha kigaidi cha Daesh kimeathirika vibaya katika kila upande.
Katika mashambulizi hayo ya anga zaidi ya magaidi 100 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ikiwemo makamanda kadhaa wa kikundi hicho wameangamizwa.
Aidha shambulio hilo limefanywa baada ya vyombo vya ulinzi vya Iraq kukusanya ripoti nzito muhimu kuhusu maeneo wanayokuwepo kikundi hicho cha kigaidi, ambapo walifahamu makazi yao muhimu yaliopo sehemu ya “Alqaimu, Akashati, Anah, Raawah na Hadilatul Ratbah” katika mkoa wa Anbar.
Mashambulio hayo yaliofanywa katika makazi ya wanajeshi wa Daesh pia yamesababisha kuangamiza kwa idadi kubwa ya silaha, vifaa muhimu na mabomu yakutengeza kwa mikono katika maeneo hayo.
Sehemu kubwa ya mkoa wa Anbar iliopo magharibi mwa Iraq iko chini ya majeshi ya Iraq na nguvu za wananchi wa nchi hiyo, ama magaidi wa Daesh wako katika maeneo ya mipakani katika mkoa huo.   
mwsho wa Habari/290